January 22, 2016


Kiungo Haruna Niyonzima anatarajia kuanza mazoezi leo baada ya uongozi kukubaliana na uongozi ambao umemsamehe baada ya kuomba radhi.

Niyonzima anatarajia kuanza mazoezi leo kwenye Uwanja wa Boko ambako Yanga itakuwa inajifua chini ya Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm ambaye amesema atampokea kiungo huyo kwa mikono miwili, atazungumza naye kabla ya kuanza kazi pamoja.

Niyonzima alisimamishwa na klabu hiyo kutokana na utovu wa nidhamu na baadaye ikatangazwa kuwa mkataba wake umevunjwa, lakini hivi karibuni aliomba msamaha na kuna taarifa kuwa ameshasamehewa na uongozi wa timu hiyo.

“Mimi sina shida na Niyonzima, ni mchezaji wangu na alikuwa anafanya vizuri sana kwa kipindi chote alichokaa hapa klabuni.

“Nipo tayari kufanya naye kazi kama atakuwa amemalizana na uongozi masuala yake ya utovu wa nidhamu, nitakachofanya ni kukaa naye chini na kuongea naye ili asirudie tena, lakini hakuna kizuizi chochote kwangu,” alisema Pluijm raia wa Uholanzi.


Taarifa zimekuwa zikisema kuwa kiungo huyo ameshamalizana na uongozi wa Yanga na kuna uwezekano mkubwa sana akaanza mazoezi na timu hiyo siku chache zijazo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic