January 22, 2016


Unaweza kudhani ni utani, lakini ukweli ni kwamba kati ya Waivory Coast wanaocheza soka hapa nchini ni Pascal Wawa (Azam FC) na Vincent Angbani (Simba) wanaojulikana kuwa wanacheza soka Tanzania, lakini upande wa mwenzao fowadi wa Azam, Kipre Tchetche kuna kitu ambacho kinashangaza kidogo.

Kwa hapa nchini Kipre ni staa mkubwa tangu mwaka 2011 alipojiunga na timu hiyo na ndiyo maana ndiye straika anayelipwa fedha ndefu zaidi nchini akipokea dola 12,000 (Sh milioni 24) kwa mwezi.
AGBANI AKIWA NA KOCHA WA AZAM FC, STEWART HALL NA KIPRE BOLOU NA BRIAN MAJEGWA WAKATI AKIWA AZAM FC

Angbani amesema kuwa utapotea njia iwapo utafika Ivory Coast na kuulizia kina Tchetche kwani hawajulikani, zaidi ya umaarufu wao kuishia kwa majirani zao tu.

“Mara ya kwanza nilishangaa sana kukuta Kipre ni staa kiasi hiki hapa Bongo, ujue kwetu tofauti na majirani hakuna anayejua kuwa anacheza soka huku, wao wanamjua Wawa na mimi,” alisema kipa huyo.


Akifafanua zaidi alisema umaarufu wake na Wawa ni kutokana na kuwahi kuichezea timu ya taifa ya vijana ya nchi yao.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic