Mshambuliaji wa Klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta, amefanikiwa kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ambapo amekuwa ni mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kufanya hivyo.
Samatta ambaye pia ni mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufanikiwa kufunga mabao nane katika mechi alizocheza huku akifunga katika mechi zote mbili za fainali dhidi USM Alger ya Algeria, ameweka rekodi hiyo ambayo imezidi kulitangaza zaidi soka la Tanzania.
Licha ya mafanikio ya tuzo hiyo, lakini inaonekana kuwa straika huyo alianza kujitambua mapema kwani ameonekana kuwa mtu mwenye mafanikio makubwa nje ya uwanja kutokana na vitu anavyomiliki.
Nyumba:
Samatta anamiliki nyumba tano ambazo zote zipo Mbagala jijini Dar es Salaam.
Kibada:
Samatta ana nyumba kubwa eneo la Kibada jijini Dar es Salaam, lakini imeanza kubomolewa na ameanza kuitengeneza upya kwa kile anachodai kuwa fundi aliitengeneza chini ya kiwango.
Kwa maelezo ya baba yake hii ndiyo nyumba anayopanga kuishi mwenyewe baada ya kuachana na soka.
Maji Matitu:
Nyumba ya pili ya Samatta ipo Mbagala Maji Matitu, hii aliinunua na kuifanyia ukarabati mkubwa.
Kiburugwa Shimo la Mchanga:
Huku ndipo ilipo nyumba ya tatu ya staa huyo wa zamani wa Simba, imeshakamilika tayari kwa matumizi.
Mbande:
Nyumba ya nne ya Samatta ipo eneo la Mbande jijini Dar es Salaam, ni nyumba kubwa, ipo eneo alipozaliwa.
Mbagala Saku:
Huku Samatta alinunua nyumba kubwa, lakini ameivunja na sasa ana mpango wa kujenga msikiti baada ya kusaini mkataba wake na Genk ya Ubelgiji.
Magari:
Kwa upande wa magari straika huyo anamiliki magari saba kama ifuatavyo.
Toyota Mark X:
Samatta anamiliki gari hili ambalo analitumia kwa ajili ya kutembelea yeye mwenyewe.
Vanguard:
Hili ni gari lake la pili ambalo anamiliki, lakini amempa mchumba wake anayejulikana kwa jina la Fatuma Omari, ndiye analitumia.
Chrysler Crossfire:
Gari hili limepaki tu nyumbani kwa Samatta kwa ajili ya dharura yoyote inayoweza kutokea.
Toyota Pajero:
Hili ni gari la kwanza kumilikiwa na mchezaji huyo mara baada ya kusajiliwa na Simba mwaka 2010, kwa sasa amempa kaka yake ndiye analitumia.
Verossa:
Gari hili Samatta ameamua kumuachia baba yake mzazi, Mzee Ally Samatta kwa ajili ya matembezi yake.
Range Rover:
Hili ni gari la kifahari ambalo Samatta ameliweka kwa meneja wake, Jamal Kisongo, amekuwa halitumii mara kwa mara.
0 COMMENTS:
Post a Comment