January 18, 2016


Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, ameamua kuvunja ukimya na kuwaambia mahasimu wao Simba kuwa itakuwa ngumu kwao kufanikiwa kutokana na timuatimua yao ya benchi la ufundi kila mara.

Kerr, raia wa Uingereza pamoja na Mkenya, Idd Salim, aliyekuwa kocha wa makipa, walifutwa kazi klabuni hapo wiki iliyopita kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mwenendo mbovu wa timu hiyo.

Lakini kwa kipindi cha miaka sita tangu mwaka 2010, Simba imeshabadilisha makocha mara 11, huku wengi wao wakikaa kwa nusu msimu tu.

Pluijm amesema anafahamu kwamba Simba ni timu kubwa kama ilivyo Yanga lakini kwa upande wake kulingana na ilikotoka timu hiyo, huu ulikuwa ni muda sahihi zaidi kumpa nafasi Kerr kuendelea kuiweka sawa timu hiyo, kwa maana haikuwa na matokeo mabovu ya kusababisha wafukuze kocha.

KERR NA IDDI

Alieleza zaidi kuwa, kama hali hiyo itaendelea, basi itakuwa ngumu kwa Simba kusimama mapema zaidi, maana wachezaji watakuwa wanayumbishwa na kuanza upya kila wakati kwa mifumo, maono, staili na falsafa tofauti za makocha wapya wanaoibuka kila baada ya kipindi kifupi.

“Nafahamu Simba ni timu kubwa na inataka irudi kwenye nafasi yake lakini nafikiri haikuwa sahihi kumuondoa Kerr wakati huu, ilikuwa ni nafasi ya pekee kwa Kerr kuendelea kuisuka Simba kwa maana haikuwa na matokeo mabovu ya kusababisha kumuondoa kocha.

“Ila kama mtindo huu utaendelea wa kufukuza benchi la ufundi kila baada ya muda mfupi, sidhani kama Simba itakaa sawa hivi karibuni, maana huwasaidii wachezaji ila unawavuruga kila mara kuwaletea mifumo, maono, staili na hata falsafa mpya kutoka kwa makocha wapya, kwa hiyo wao kila siku wanakuwa ni watu wa kuanza upya,” alisema Pluijm aliyeiongoza Yanga kutwaa ubingwa wa 25 msimu uliopita.


Kerr ameiacha Simba kwenye nafasi ya tatu baada ya kuiongoza katika mechi 13 za Ligi Kuu Bara ambazo ilishinda nane, sare tatu na kufungwa mbili na kukusanya pointi 27, ikiwa tofauti ya pointi sita dhidi ya Yanga.   

1 COMMENTS:

  1. Kwa sababu timu yake iko vizuri ndio maana anaropoka hayo. Kwa lengo la simba kuendelea kuwa mdebwedo. Ukichukua kiwango cha mchezaji mmoja mmoja simba na mtibwa. Utakubaliana na mimi kuwa simba ina wachezaji wazuri. Tazizo simba haina mpango mzuri wabkutafuta goli. Utaona kila mechi na kila goli la simba ni uwezo wa mchezaji. 2 Simba haicheji kitim kila mchezaji anacheza kwa mipango yake.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic