January 18, 2016


Baada ya kuwa nje kwa wiki nzima, kiraka wa Yanga, Mbuyu Twite, anatarajiwa kuanza mazoezi leo lakini kwa upande wa nahodha wa kikosi hicho, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, bado haijaeleweka anarejea lini uwanjani.

Cannavaro hajakanyaga uwanjani tangu acheze mchezo wa marudiano wa timu ya taifa, Taifa Stars dhidi ya Algeria ugenini ambao Stars ililala mabao 7-0 ambako aliumia mfupa wa kisigino.

Twite aliumia kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi wiki mbili zilizopita, lakini leo huenda akaanza mazoezi ya jumla na wenzake.

Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya, amesema hajajua ni lini Cannavaro atarejea uwanjani, kwani wanasubiri majibu ya daktari wa mifupa Muhimbili ili kujua tatizo lake litamchukua muda gani.

Aliongeza kuwa, wamelazimika kumfunga hogo (P.O.P) jingine baada ya lile la awali lililokuwa litolewe baada ya wiki tatu, hata hivyo mfupa ulikuwa haujaunga.

“Mpaka sasa hakuna mwenye jibu kamili Cannavaro anarudi lini uwanjani lakini inaweza kumchukua muda maana tulilazimika kumfunga P.O.P nyingine baada ya kukuta mfupa wa kisigino haujaunga. 

Tunasubiri majibu ya daktari wa mifupa Muhimbili, alikuwa atupe jibu juzi lakini kwa siku mbili mfululizo amekuwa ‘bize’ sana, hivyo mpaka kesho (leo),” alisema Matuzya na kuthibitisha Twite kurejea uwanjani.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic