February 4, 2016


Kikosi cha Abajalo ya Sinza inayoshiriki daraja pili kiko katika hali ngumu baada ya kuandamwa na ukata.

Katibu Mkuu wa Abajalo, Novatus Damian amesema wako katika hali ngumu ya kifedha, hali inayowafanya kulazimika kuwaomba wadau mbalimbali wa Sinza na wapenda michezo nchini kote kuisaidia.

“Tuko katika hatua ya mwisho ya ligi daraja la pili, tumebakiza mechi nne. Kesho tunacheza dhidi ya Mshikamano, tunaona chonde watusaidie.

“Ni masuala ya posho za wachezaji, usafiri na mambo mengine madogomadogo. Tafadhari wajitokeze kwa kuwa kama tutafanya vizuri katika mechi hizo tutarejea ligi daraja la kwanza,” alisema Damian maarufu kama Tusi.

Abajalo inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mashujaa, Sinza jijini Dar es Salaam na Tusi alisema anapatikana kwa namba 0714894310.

Kikosi cha Ajabalo linasifika kwa kutoa wachezaji wengi nyota kama vile Kalimangonga ‘Kally’ Ongala, Lucas Matokeo, George Ngasongwa, Edward Kayoza, Raymond Ndunguru ‘Okocha’ pia Aaron Nyanda na Ally Mayay ‘Tembele’ walipitia hapo.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic