UGANDO AKIPAMBANA KATIKA MECHI DHIDI YA MGAMBO... |
Na Saleh Ally
Kati ya wachezaji walioonyesha kiwango kizuri baada ya kupewa nafasi Simba ni Hija Ugando.
Kocha Jackson Mayanja amekuwa mwepesi kung’amua kwamba mchezaji huyo kinda ana uwezo na anastahili kupata nafasi.
Katika mechi tatu, Ugando amefunga bao moja lakini akaonyesha uwezo mzuri kwa kipimo cha mchezaji kinda.
Ili afanikiwe na kutimiza malengo ya pande zote mbili, yaani yeye na upande wa kocha ni lazima kila upande uwe na tamaa ya kutouangusha upande mwingine.
Ugando lazima asivimbe kichwa, ahakikishe anatimiza malengo kwa kufanya vizuri kwa faida yake na Simba.
Kwa upande wa Mayanja kwa kuwa ameamua kumpa Ugando nafasi, lazima akubali kwamba kukosea ni kujifunza hata kama kuna kipimo chake.
Hivyo anachotakiwa ni kumpa nafasi tena na tena kadiri inavyowezekana ili aendelee kupata uzoefu na kujenga hali ya kujiamini.
Kocha Dylan Kerr alimuamini Ugando, lakini hakumoa nafasi ya kutosha sana. Mayanja amemuamini zaidi na mabadiliko makubwa yanaonekana kwa Ugando.
Ugando ana nguvu ingawa lazima aongeze mazoezi, ana kasi na mwepesi wa maamuzi. Akiendelea kupata nafasi ajiamini, kupata nafasi ajifunze basi Simba itapata faida kubwa hapo baadaye.
0 COMMENTS:
Post a Comment