Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema katika kikosi chake kuna mambo ya kurekebisha, lakini anaamini Yanga itarejea katika kiwango kizuri na kuendelea kufanya vizuri.
Yanga imepoteza mechi yake ya kwanza kwa mabao 2-0 ikicheza na Coastal Union kabla ya kuambulia sare ya mabao 2-2 dhidi ya Prisons mjini Mbeya, jana.
Pluijm raia wa Uholanzi, amesema nafasi ya kufanya vema zaidi ipo kwa kuwa wana kikosi bora.
Lakini akasisitiza, ili waendelee kufanya vizuri yako mambo kadhaa muhimu ya kufanya ukiwepo utulivu.
“Mechi za mikoani ni ngumu sana, umeona mazingira yanavyokuwa tofauti kabisa na Dar es Salaam.
“Kiwanja ni moja ya vikwazo, lakini tuna kikosi bora na tuna nafasi ya kufanya vema tena.
“Kikubwa ni utulivu, nimezungumza na wachezaji na kuwahimiza kujituma zaidi lakini suala la utulivu ni muhimu sana,” alisema.
Pluijm alisema wataendelea kurekebisha mambo mengine ambayo wanayaona ni sehemu ya marekebisho ya mchezo.
0 COMMENTS:
Post a Comment