February 8, 2016


Wakati Simba ikiwa kwenye moto wake, ghafla kumeibuka taarifa ya kutakiwa kwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Mwinyi Kazimoto na timu ya Al Markhiya ya Qatar aliyokuwa akiitumikia awali.

Taarifa zinaeleza kuwa hii ni mara ya pili sasa tangu kuanza kwa msimu wa 2015/16 Waarabu hao wanajaribu kuleta ofa hiyo juu ya mchezaji huyo baada ya uongozi wa Simba kuikataa ile ya awali iliyokuja mwanzoni mwa msimu huu.

Kazimoto alitimkia Al Markhiya kwa mara ya kwanza mwaka 2012 akitokea Simba SC kabla ya kurejea nchini mwaka jana ikielezwa kuwa ameachwa na timu hiyo kutokana na sheria mpya za shirikisho la nchi hiyo kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni.


Hata  hivyo, baada ya tathmini ya mechi zake, benchi la ufundi la timu hiyo limegundua kuwa viungo wapya walioko katika kikosi hicho hawakidhi kama ilivyokuwa kwa Kazimoto, hivyo wamewasilisha tena ombi lao wakitaka Simba iwasikilize.

“Ndiyo, wale jamaa wa Markhiya wanamtaka tena Mwinyi kwa kigezo kuwa uwezo wake ulikuwa mkubwa zaidi ya viungo waliopo hapo kwa sasa, hii ni mara ya pili kuleta ombi hilo tangu kuanza kwa msimu huu, mara ya kwanza walimtaka tukawagomea lakini sasa wamerudi tena,” alisema moja ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo.

Alipotafutwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe kulitolea ufafanuzi suala hilo, alisema: “Hizo taarifa kama zipo basi hazijafika kwangu, siwezi kusema lolote kuhusu Kazimoto mpaka nipate hizo taarifa na itahitajika makubaliano ya wote kabla ya kuamua kumuuza au la.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic