February 8, 2016


Mambo yakikaa sawa basi baada ya miezi michache mno, Simba itakuwa na uwanja wake bomba wa mazoezi wenye kiwango kizuri kwa ajili ya kujifua na michuano mbalimbali.
Iko hivyo kwa kuwa wiki iliyopita tayari uongozi wa Simba umefanya mawasiliano na moja ya kampuni za nchini China na kuwapa oda ya kuwatengenezea nyasi bandia ‘kapeti’ kwa ajili ya uwanja wao uliopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar.

Tayari kila kitu kimekamilika na kampuni hiyo imewaeleza kwamba takriban baada ya wiki tatu kila kitu kitakuwa tayari na mzigo utatumwa mapema mno.

Wakati hayo yakiendelea juzi Jumamosi, Rais wa Simba, Evans Aveva na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, walikwenda kutembelea kiwanja hicho kuangalia kinachoendelea baada ya kuamuru kufanyika kwa matengenezo ya awali kwa kuuweka sawa udongo huo wa uwanjani hapo kisha mengine yafuate.

“Tumeshaagiza hizo nyasi na kila kitu kinakwenda sawa, kwa kuanzia ni kutafuta ‘pitch’ ya kuchezea kwanza kisha mengine kama uzio yatafuata. Baada ya kufika kwa nyasi, utengenezwaji na uwekwaji wa nyasi hizo huchukua kama siku sita mpaka 10.


“Kwa hiyo kwa mahesabu hayo unaweza kuona inaweza kuchukua kama mwezi na nusu hivi na tunayoyapanga yakakaa kama tunavyotaka,” alisema Hans Poppe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic