Kikosi cha Simba kimeindoka jijini Dar es Salaam leo alfajiri kwenda mkoani Shinyanga kwa ajili ya mechi yake ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagare Sugar.
Simba wameondoka na basi lao wakiwa na kikosi kamili kasoro mshambuliaji Paul Kiongera ambaye ni majeruhi na amerejea kwao Kenya kujiuguza.
Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema safari hiyo imeanza mapema kwenda kupambana tena mjini Shinyanga.
Mechi hiyo itapigwa keshokutwa Jumamosi kwa kuwa Kagera Sugar imeamua kuuhama Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora na kurejea Shinyanga. Hii inatokana na Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kuwa kwenye matengenezo makubwa.
"Baada ya kazi moja, inafuata nyingine. Tumeanza safari ya kwenda Shinyanga, tunaomba dua zenu," alisema Manara.
Simba inakwenda Shinyanga baada ya kuwa imetoa kipigo cha mabao 5-1 kwa Mgambo Shooting ya Tanga, jana.
0 COMMENTS:
Post a Comment