February 4, 2016



FREDERICK MWAKALEBELA

Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Frederick Mwakalebela amelalamika kuhusisha na sakata la beki wa zamani wa Yanga, David John Mwakalebela ambaye amepandishwa kuzimbani.

Hii hapa kauli ya Mwakalebela mwenyewe....

"Kumekuwa na upotoshaji wa taarifa zinazosambaa juu ya David Mwakalebela, baadhi ya vyombo vya habari yaani magazeti na mitandao ya kijamii vimekuwa vikielekeza tuhuma hizo dhidi yangu kwa makusudi au kwa kutokujua jambo ambalo ni hatari kwa Mimi binafsi, familia na marafiki kwa ujumla.

DAVID MWAKALEBELA

Aidha, napenda umma wa Watanzania utambue kuwa Mimi ni Fredrick Wilfred Mwakalebela na mtuhumiwa ni David John Mwakalebela ambaye amewahi kuwa mchezaji wa Yanga na timu ya taifa 'Taifa Stars', wakati Mimi Fredrick Wilfred Mwakalebela nilikuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe.

Aidha, napenda kuwapa pole wanafamilia yangu, ndugu, jamaa na marafiki kwa usumbufu wote uliojitokza kwao kutokana na sintofahamu hii na kusababisha kadhia dhidi yako.


Mimi Fredrick Wilfred Mwakalebela

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic