Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo amesema kwamba pamoja na kuwa muumini wa kuwatetea waamuzi, lakini wamuzi aliyewachezesha mechi yao dhidi ya African Sports, anapaswa kulaumiwa.
Mwadui FC imekutana na kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa African Sports 'Wana Kimanukanu' kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, jana.
Kihwelo maarufu kama Julio amesema amekuwa akiwatetea sana waamuzi katika masuala ya uchezeshaji.
“Lakini aliyetuchezesha sisi, alionyesha wazi hakutaka tushinde. Haikuwa sawasawa, pia ninashauri hakika waamuzi wanapaswa kutenda haki,” alisema Julio.
Pamoja na kipigo hicho Mwadui FC imeendelea kubaki katika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya Yanga, Simba, Azam na Mtibwa Sugar.
0 COMMENTS:
Post a Comment