Wengi waliamini Arsenal haina ubavu wa kuizuia Barcelona katika mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Emirates jijini London, leo.
Kweli wamepatia, kwani Arsenal imelazwa kwa mabao 2-0 huku ikihenyeshwa kwa kiasi kikubwa uwanjani.
Lionel Messi ndiye alifunga mabao hayo mawili katika kipindi cha pili, akianza na lile la kwanza katika dakika ya 71 baada ya kupokea pasi safi ya Neymar aliyeambaa pembeni mwa uwanja kwa kasi.
Messi tena, aliangushwa na mwamuzi Cuneyt Cakir kutoka Uturuki, akaamuru ipigwe penalti. Messi hakufanya ajizi, akaikwamisha wavuni katika dakika ya 84.
Dakika tatu baadaye, kipa Petr Cezch wa Arsenal akafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa kichwa wa Neymar.
Katika kipindi cha kwanza, Arsenal walipoteza nafasi tatu za kufunga ambazo zinegeweza kubadilisha mambo. Hata hivyo wachezaji wake walionekana kama ni wenye hofu na walioshindwa kufanya mambo kwa uhakika.
Kama wangekuwa watulivu, huenda wangepusha kunyanyaswa muda mrefu na Barcelona walioonekana kama wako nyumbani.
0 COMMENTS:
Post a Comment