February 24, 2016


Pamoja na kuanza kwa kufunga mabao mawili, Bayern Munich imeshindwa kuyalinda baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 ikiwa ugenini dhidi ya Juventus ya Italia.

Mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ilikuwa tamu na ya kuvutia, Bayern ilipata mabao yake kupitia Thomas Muller katika dakika ya 43 na Arjen Robben akafunga la pili katika dakika ya 55.


Lakini wenyeji Juventus wakaendelea kuonyesha ni wabishi walipopata bao katika dakika ya 63 kupitia Paul Dyabala kabla ya Stefano Sturaro kusawazisha katika dakika ya 76.

Majibu ya nani anasonga hadi robo fainali, yatapatikana katika mechi ya pili jijini Munich, Ujerumani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic