Sijui ni dharau, au uwezo mkubwa? Kikosi cha Barcelona hakikufanya mabadiliko hata ya mchezaji mmoja katika mechi yake dhidi ya Arsenal.
Katika mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Emirates jijini London, Barcelona ilitumia wachezaji 11 tu bila kubadili hata mmoja.
Kwa upande wa Arsenal ambayo ilikuwa nyumbani, iliwatoa Alex Oxlade-Chamberlain akaingia Theo Walcott, Olvier Goroud akaingia Danny Welbeck na matheu Flamini akachukua nafasi ya Francis Coquelin.
Pamoja na kutobadili mchezaji hata mmoja, Barcelona ndiyo walioonekana kutawala kila idara huku MSN yaani Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar wakifanya wanavyotaka.
0 COMMENTS:
Post a Comment