Kipa mkongwe wa Yanga, Ally Mustapha ‘Barthez’, juzi aligeuka kocha wa muda wakati timu yake ilipokuwa ikikipiga na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, hiyo ni kutokana na kuwa bize akielekeza vitu akiwa katika benchi.
Kwanza alianza kuwaelekeza wenzake wa kwenye benchi vitu fulani, baadaye alipoona mambo hayaendi sawa alisimama na kutoa maelekezo kwa wenzake uwanjani huku makocha wake wakiwa wanajadiliana mambo.
Alikuwa akifanya hivyo baada ya kuona muda unakwenda na Yanga ikiwa nyuma.
Huenda hofu yake kubwa ilikuwa ni wao kupoteza mechi kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuwa wamefungwa kwa mabao 2-0 na Coastal Union mjini Tanga.
Baadaye alirudi katika benchi na kuacha kazi hiyo ya maelekezo ikitolewa na makocha wake, hata hivyo matokeo ya mchezo huo wa Ligi Kuu Bara yalikuwa ni sare ya 2-2.
0 COMMENTS:
Post a Comment