Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm amesema makosa yaliyofanywa na safu yake ya ulinzi katika mechi mbili zilizopita ndiyo yaliyotibua mipango yake.
Katika mechi hizo mbili zilizopita, Yanga imecheza dhidi ya Coastal Union na Prisons ambapo ilifungwa mabao 2-0 kisha sare ya 2-2, huku mabeki wa kati wakionekana kutokuwa makini.
Tangu nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aumie miezi miwili iliyopita, safu ya ulinzi ya Yanga imekuwa ikiundwa na Vincent Bossou na Kelvin Yondani huku Yondani naye akikosa mechi ya Prisons kutokana na kuwa na kadi nyekundu.
Pluijm amesema wapinzani wao wamekuwa wakiwakamia lakini makosa ya mabeki wake yamechangia kufungwa.
“Wapinzani wamekuwa wakitukamia sana, hali kama hii huwa inatokea kwa timu yoyote ile hata Ulaya na si kwa Yanga pekee. Pia kulikuwa na makosa kadhaa, nitayarekebisha,” alisema Pluijm.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment