February 5, 2016


Katika kuhakikisha anarejea kwa haraka uwanjani ili kuiokoa timu yake, nahodha na beki wa kati tegemeo wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ameongeza muda wa kujifua kwa ajili ya kujiweka fiti na ikiwezekana kucheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba mnamo Februari 20, 2016.

Cannavaro ameongeza dozi ili kurejea katika kikosi cha kwanza baada ya kuwa nje kwa muda mrefu huku kocha wake, Hans van Der Pluijm akisikika akilalamika mara kadhaa juu ya safu yake ya ulinzi kulega katika mechi za hivi karibuni.

Tangu awe majeruhi, nafasi ya Cannavaro imekuwa ikimilikiwa na Mtogo, Vincent Bossou ambaye pia amekuwa akipewa kitambaa cha unahodha katika baadhi ya mechi.


 Cannavaro alisema hivi sasa anafanya mazoezi kwa saa tatu, wakati anaanza mazoezi hayo alianza kwa kufanya kwa saa mbili.

Mazoezi anayofanya zaidi ni ya gym lengo likiwa ni kuongeza ufiti pamoja na pumzi ili atakapoanza mazoezi ya uwanjani, awe fiti kwa ajili ya mapambano.



“Ninataka kabla ya mechi ya Simba niwe fiti kabisa kwa ajili ya mapambano, ndiyo maana nimeanza mazoezi magumu ya gym yaliyolenga fitinesi ili nitengeneze fiziki, stamina na pumzi,” alisema Cannavaro. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic