February 13, 2016

NAY

Baada ya kuzua sekeseke, Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limeufungia rasmi Wimbo wa Shika Adabu Yako ulioimbwa na msanii Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili.

Basata imesema wimbo huo umefungiwa kwani una kashfa, uchochezi, kudhalilisha watu na kuhatarisha amani na utengamano miongoni mwa wasanii na jamii kwa ujumla.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza, sambamba na kuufungia wimbo huo, baraza litampa karipio kali msanii huyo na kumtaka kutoendelea kuusambaza zaidi.  

“Kifungu cha 4 (1) (j) cha sheria ya Basata namba 23 ya mwaka 1984, Baraza lina mamlaka ya kuratibu na kufuatilia mienendo ya mtu yeyote anayejihusisha na sanaa na kuhakikisha linalinda maadili ya kitaifa miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya sanaa.

“Aidha, kifungu cha 4 (2) cha sheria hii kinalipa baraza nguvu ya kisheria kufanya jambo lolote lile kuliwezesha kufanya majukumu yake kwa faida na ustawi wa taifa,” alisema Mngereza. 

Alisema Basata imepokea maswali na malalamiko kadhaa kutoka kwa wadau wa sanaa ambao wameguswa na kuchukizwa na wimbo huo.


Juhudi za kumpata Nay wa Mitego ili aweze kuzungumzia ishu hiyo lakini simu yake haikupatikana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic