February 13, 2016




CHABRUMA (WA PILI KULIA WALIOLALA) AKIWA NA KIKOSI CHA TWIGA STARS NCHINI ETHIOPIA. KIKOSI HIKI NDICHO KILIING'OA ETHIOPIA KWAO KWA KUICHAPA MABAO 3-1 NA KUFUZU KUCHEZA KOMBE LA MATAIFA AFRIKA.

Winga wa zamani wa Twiga Stars, Ester Chabruma ameteuliwa kuwa mtunza vifaa wa kikosi hicho.

Chabruma aliwahi kubandikwa jina la Lunyamila katika miaka ya mwanzoni mwa 2000 wakati soka la wanawake linachipukia nchini.

Wakati fulani aliwahi kucheza soka barani Ulaya, lakini hakuwa na mafanikio makubwa sana.

Baadaye Asha Rashid 'Mwalala' aliyekuwa chipukizi wakati wake aligeuka na kuwa mrithi wake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic