Beki wa kushoto wa Yanga, Haji Mwinyi, ameshusha presha kwa kurejea kikosini baada ya kupona maumivu ya tumbo huku akiahidi kuwepo uwanjani katika mechi ya watani wao wa jadi Simba.
Mwingi hadi hivi sasa amekosa mechi wdhidi ya Majimaji FC waliyoshinda mabao 5-0 na nyingine ya Coastal Union iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga waliyofungwa mabao 2-0, pia dhidi ya Prisons waliyotoka sare ya mabao 2-2.
Beki huyo tangu ametua Yanga msimu huu wa Ligi Kuu Bara amejihakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, akifanikiwa kumtoa Oscar Joshua.
Mwinyi amesema kuwa amepona maumivu hayo na anatarajia kujiunga na kikosi hicho mara baada ya timu hiyo kurejea jijini Dar es Salaam ikitokea Mbeya kucheza na Prisons.
“Nimeanza mazoezi binafsi ya kujiweka fiti zaidi ili mechi dhidi ya Simba nicheze, mashabiki washushe presha, nimepona,” alisema Mwinyi.
0 COMMENTS:
Post a Comment