February 6, 2016

CHUJI

Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ hamtumii Athuman Idd ‘Chuji’ katika kikosi chake, ishu ikiwa ni moja tu, kwamba kiungo huyo anatakiwa ajitume ili apate nafasi ‘first eleven’.

Tangu Desemba mwaka jana, Chuji amekosa mechi za Mwadui na kuzua maswali mengi miongoni mwa wadau wa soka lakini Julio amesisitiza: “Siridhishwi na kiwango chake.”

Chuji sambamba na nyota wengine kutoka Simba na Yanga wakiwemo Jerry Tegete, Nizar Khalfan na Joram Mgeveke, walisajiliwa na Mwadui msimu huu ili kuiongezea nguvu timu hiyo katika Ligi Kuu Bara.

Julio amesema mchezaji anayepata nafasi ya kucheza katika kikosi chake ni yule anayeonyesha uwezo na si vinginevyo, hivyo ni sawa na Chuji ambaye hamtumii kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake.

“Kwa nini aulizwe Chuji tu wakati nina wachezaji wengi? Inawezekana siwezi kumchezesha  kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake, mpira unahitaji mazoezi, kama haupo vizuri utakaa nje.


“Hakuna nafasi kwa mchezaji asiyekuwa na kiwango, akiwa vizuri atacheza kama wachezaji wengine wanavyocheza, ukiona mtu yupo nje, ujue amezidiwa kiwango na wachezaji wengine,” alisema Julio.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic