February 6, 2016


Kiungo Said Ndemla hana nafasi kikosi cha kwanza cha Simba na mara nyingi amekuwa akiingia akitokea benchi huku Kocha Jackson Mayanja akiwatumia zaidi Jonas Mkude na Justice Majabvi.

Kutokana na hali hiyo, Ndemla amesema hatishwi na kuwekwa benchi kila mara kwani anajijua anamudu kucheza nafasi tano uwanjani na ameamua kujifua zaidi arudi first eleven.

Ndemla alisema anamudu kucheza kiungo namba sita, kiungo mashambuliaji namba nane, winga ya kulia na kushoto, hata mshambuliaji msaidizi, yaani namba 10.

“Sijui kwa nini kocha hanitumii, ila yeye ndiye anayejua mahitaji ya kikosi, mimi sihitaji kumuingilia katika hilo. Ila kwa upande wangu, kwa kuwa nacheza nafasi tano za viungo uwanjani, nitahakikisha narejea kikosini.

“Nitaongeza bidii katika mazoezi ili niweze kumshawishi kocha anipe nafasi ya kuanza kikosini, ninachotaka ni kurudi kikosini, sitajali kuhusu nafasi,” alisema Ndemla. 


Kuhusiana na hilo, Mayanja alisema: “Ndemla ni mchezaji mzuri lakini bado naendelea kumuandaa, haiwezekani wakacheza wachezaji wote, kumbuka kuna mifumo na falsafa katika soka.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic