Azam FC ni moja ya timu tishio katika Ligi Kuu Bara, lakini haikufika hapa kirahisi hata kama inamilikiwa na tajiri namba moja nchini Said Salim Bakhresa.
Mmoja wa wachezaji wanaopaswa kupewa shukurani kutokana na mchango wake ni Shekhan Rashid ambaye sasa anaendesha maisha yake katika jiji la Stockholm nchini Sweden.
Shekhan alikuwa mmoja wa manahodha wa mwanzo kabisa wa Azam FC, akiwa amerejea nchini kutoka Sweden.
Alifanya vizuri zaidi nyumbani na kimataifa akiwa na Simba SC, baadaye akaenda Sweden kabla ya kurejea na kuipa nguvu Azam FC.
Katika picha unamuona Shekhan akiwa na utepe wa nahodha, karibu yake John Bocco akiwa amemkumbatia. Kwa sasa Bocco ndiye nahodha wa Azam FC akiwa mchezaji aliyeanza na timu hiyo hadi leo.
Pia unamuona Tumba Sued, kwa sasa yuko Mbeya City lakini Nsa Job na kipa Mrundi, Vladimir Niyonkuru. Azam FC, pia imetokea mbali.
PICHA KWA HISANI YA SHEKHAN RASHID.
0 COMMENTS:
Post a Comment