MPIRA UMEKWISHA
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
DK 87 hadi 90, Yanga wanaendelea kujiamini kwa kuwa dakika zinaruhusu wao kujidai na kwamba hakuna kinachoweza tena kuwazuia kusonga mbele
Dk 85 hadi 87, Yanga wanaonekana kuutawala mchezo, wanacheza wanavyotaka lakini hawana umakini katika umaliziaji
Dk 85, MWashiuya anapiga krosi safi kwa Tambwe, akiwa yeye pekee anapiga kichwa hovyooooo na mpira unapaa
Dk 83, Msuva anapewa pasi nzuri, akiwa katika nafasi nzuri lakini anashindwa kupiga vizuri kwa mguu wa kushoto, mpira unatoka nje unakuwa fyongo kabisa
Dk 81, Tambwe na Kamusoko wanaingia vizuri eneo la hatari, lakini beki Nadrii wa Cercle de Joachim anaokoa vizuri kabisa katikati yao
Dk 79, Mwashiuya anamchambua beki mmoja wa Cercle de Joachim na kupiga krosi nzuri, lakini Tambwe anateleza wakati akienda kufunga, mabeki wanaosha
SUB Dk 77 Cercle de Joachim wanamuingiza Jack Daniel kuchukua nafasi ya Wing
Dk 76, Tambwe anaruka juu kupiga kichwa, anafanikiwa kuiwahi krosi ya Juma Abdul lakini anashindwa kulenga lango
SUB Dk 75, Kaseke anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Geofrey Mwashiuya
Dk 74, Juma Abdul anapanda lakini beki wa Cercle de Joachim anaokoa na mpira kuwa kona. Inachongwa na Msuva, anaichonga vizuri katikati ya lango lakini Issack anaokoa.
Dk 73, Yanga wanafanya shambulizi kubwa, Mwinyi Haji anagongeana vizuri na Kaseke, anaingia na kupiga krosi ya chini. Tambwe anauwahi mpira na kupiga shuti lakini kipa Cercle de Joachim anaokoa. Kipa huyo analala chini ameumia, hata hivyo anaamka na mpira unaendelea
Dk 67, Msuva anapata pasi nzuri ya kichwa kutoka kwa Tambwe, lakini anashindwa kulenga lango. Kipa wa Cercle de Joachim anaonekana kuwalaumu mabeki wake
Dk 64, Kaseke anapokea pasi nzuri nje ya 18, anapiga shuti kali kabisa lakini mpira unawababatiza mabeki wa Cercle de Joachim na kuokolewa
Dk 57 hadi 61, Yanga wanaonekana kucharuka na kushambulia kwa kasi zaidi, hata hivyo safu ya ulinzi ya Cercle de Joachim wanaonekana kuwa makini
GOOOOOOO Dk 56, Kamusoko anawafungia Yanga bao la pili kwa mkwaju safi wa faulo baada ya Msuva kumuachia mpira Haji Mwinyi, aliyempasia mfungaji akaachikia kiki takribani mita 21 nje ya lango.
Dk 53, Msuva tena anafanikiwa kupata nafasi nyingine, lakini naye anapiga nje mpira huo
DK 52, nafasi nzuri kabisa kwa Nonga akiwa na kipa lakini anashindwa kutulia, hili lingekuwa ni bao la pili la Yanga
DK 46, Yanga wanamtoa Busungu na nafasi yake inachukuliwa na Paul Nonga, Twite pia anakwenda nje, anaingia Pato Ngonyani
MPIRA MAPUMZIKO
Dk 45, Yanga wanapata kona, lakini kipa wa Cercle de Joachim anaonyesha umahiri na kudaka vizuri kabisa
Dk 43, Busungu tena, yeye na kipa lakini anashindwa kuuguka mpira uingie wavuni
Dk 38, Yanga wanapata nafasi nyingine, lakin wanashindwa kuitumia. Krosi nzuri lakini Busungu anapiga kichwa cha kuparaza na mpira unatoka nje
Dk 37 Cercle de Joachim wanaata kona baada ya Bossou kuutoa mpira nje. Hata hivyo wanapiga kona dhaifu ambayo Yanga wanaokoa kwa ulaini
Dk 32 hadi 36, bado Yanga wanaonekana kutawala mpira hasa katika sehemu ya kiungo. Lakini bado mipango yao haina uhakika
Dk 31 Yanga wanapata nafasi nyingine, lakini Tambwe anashindwa kupiga akiwa katika nafasi nzuri kabisa katika lango la Cercle de Joachim
Dk 28, pasi ya Kaseke, linamkuta Juma Abdul anapiga shuti kali kabisa lakini anashindwa kulenga lango
Dk 26, Yanga inapata kona baada ya krosi ya Msuva kuokolewa. Mpira unatua kwenye kichwa cha Bossou lakini ni goal Kick
Dk 24 Bado Cercle de Joachim wanaendelea kubaki katika eneo la zone yao. Lakini inaonekana wanajua wanachokifanya. Tatizo la Yanga linaonekana kuwa ni mipango ya mwisho kila wanapofika katika lango la wapinzani wao
Dk 19 hadi 22, Yanga ndiyo wanaonekana kumiliki mpira zaidi, kiungo Thabani Kamusoko anaonekana kama yuko mwenyewe, anafanya anavyotaka huku Cercle de Joachim wakiwa wamejazana nyuma ya mpira
Dk 18, Cercle de Joachim wanafanya shambulizi jingine la kushitukiza, lakini Yondani anakuwa mwepesi kuwahi na kuokoa mpira
Dk 9 hadi 12, Yanga wanaonekana kushambulia zaidi huku wakitawala katika nafasi ya kiungo huku Cercle de Joachim wakijilinda zaidi
Dk 8 Busungu anaingia vizuri baada ya mabeki wa Cercle de Joachim kudhani ameotea, lakini anashindwa kulenga lango
Dk 6, Sherve anaingia vizuri na kupiga shuti linapita juu kidogo ya lango la Yanga
GOOOOOOOOOO Dk 3, krosi safi ya Simon MSuva, Tambwe anaruka na kupiga kichwa safi kinachotikiza nyavu
Dk 2, Emerson wa Cercle de Joachim anaingia vizuri, anawazidi mbio akina Bossou lakini kipa Barthez anatoka na kuokoa
Dk 1 Msuva anaingia kazi katika lango la Cercle de Joachim lakini kipa wao anatoka na kuokoa
KIKOSI
1. Ally Mustapha 'Barthez'
2. Juma Abdul
3. Haji Mwinyi
4. Kelvin Yondani
5. Vicent Bossou
6. Mbuyu Twite
7. Simon Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Amissi Tambwe
10. Malimi Busungu
11. Deus Kaseke
Sub:
12. Deo Munishi
13. Oscar Joshua
14. Pato Ngonyani
15. Matheo Simon
16. Paul Nonga
0 COMMENTS:
Post a Comment