Mpira umekwisha na Prisons imeing'oa kwa mabao 2-1 na sasa inasonga robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD.
Mechi hiyo imepigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na haikuwa na mashabiki wengi sana kutokana na mvua kali iliyonyesha kuanzia asubuhi hadi mchana.
**************
Dk 83 Hannington Kasubula anafanya kosa baada ya kuukosa mpira aliotaka kuudaka, mpira unadunda na kwenda wavuni, Prisons inatapa bao la pili.
Ulikuwa mpira dhaifu kabisa ambao ulikuwa kama kiungo mmoja wa Prisons akiwa ameokoa.
Dk 47, Joseph Mahundi anaisawazishia Mbeya City kwa shuti la kuchumpa baada ya kupata krosi nzuri kabisa ya Haruna Moshi 'Boban'
Mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya wapinzani wakubwa wa jiji la Mbeya, yaani Prisons na Mbeya City inaendelea.
Hadi sasa, Prisons wanaongoza kwa bao moja walilolipata katika dakika ya 38 kupitia Mohmmed Mkopi, aliyeunganisha mpira wa adhabu kwa kichwa.
Wachezaji wa timu zote wanapambana ila mpira unaonekana kuwa mgumu kutokana na mvua kubwa iliyonyesha leo mjini Mbeya.
0 COMMENTS:
Post a Comment