February 12, 2016

MWESIGWA
Taarifa ni kuwa hali si shwari ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), inaonekana kama kuna utulivu lakini nyuma ya pazia kuna tetesi kuwa wafanyakazi wa taasisi hiyo hawajalipwa mishahara kwa muda wa miezi miwili mfululizo sasa.

Habari kutoka ndani ya TFF ambayo inaongozwa na Jamal Malinzi ni kuwa malimbikizo ya mishahara yalianza tangu Desemba, mwaka jana na hata mshahara wa Novemba, mwaka jana walilipwa mwisho wa Januari, mwaka huu.

“Haieleweki hapa, hakuna mishahara kwa miezi miwili mfululizo sasa, huo wa Novemba, mwaka jana ndiyo umetoka mwisho wa mwezi wa Januari. Hatujajua inakuwaje kwa kweli,” alisema mtoa taarifa huyo.

“Maisha ni magumu, hakieleweki na jamaa naona wanapita tu hapa. Pia hakuna maelezo ya kutosha au ufafanuzi ambao ungefanya watu wajue nini cha kufanya,” kilieleza chanzo.

Alipotafutwa Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa ambaye baada ya kuelezwa juu ya tuhuma hizo alionyesha kutokuwa tayari kulitolea ufafanuzi suala hilo.

“Hayo ni masuala ya utawala, siwezi kuyatolea ufafanuzi. Mambo ya maslahi ni baina ya mwajiri na mwajiriwa, sasa siwezi kuanza kuyazungumzia au kuyatolea ufafanuzi wowote,” alisema Mwesigwa na kukata simu.


SOURCE: CHAMPIONI 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic