February 16, 2016


Kocha wa Simba, Jackson Mayanja amesema kikosi chake kinalenga kupata pointi tatu kutoka kwa Yanga, Jumamosi.
Mayanja amesema Simba haitaenda uwanjani kwa lengo la kulipa kisasi, badala yake ni pointi tatu.

Ukiangalia kitu muhimu kabisa ambacho tunakihitaji Jumamosi ni pointi tatu kwa ajili ya kupigania ubingwa. 

Suala la kisasi kwa kuwa Simba ilifungwa mechi ya kwanza si muhimu sana,” alisema Mayanja.

“Wachezaji wanajua, tumejiandaa kwa lengo la kupambana, kuhakikisha tuko katika hali nzuri.”


Katika mechi ya mzunguko wa kwanza, Simba ilifungwa kwa mabao 2-0, jambo ambalo Wanamsimbazi wengi wangetaka kuona, kisasi kinalipwa.

1 COMMENTS:

  1. mayanja kaongea point ambayo wangeenda kulipa kisasi wangepigwa nyingi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic