Kocha mahiri wa makipa, Haroon Amur Al Siyabi ameanza kazi ya kuwanoa makipa wa Simba, siku chache kabla ya mechi dhidi ya Yanga.
Al Siyabi alianza kazi hiyo jana katika kambi ya Simba, nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Kocha huyo wa timu za taifa za Oman ni mkufunzi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), amekuwa akija nchini mara kwa mara kuwanoa makipa wa Simba.
Taarifa zinaeleza aliwasili nchini wiki iliyopita lakini Simba ilikuwa mjini Shinyanga ikipambana ambako ilifanikiwa kubeba pointi sita kwa kuzitwanga Kagera Sugar na Stand United.
AKIMNOA IVO MAPUNDA WAKATI AKIWA SIMBA MWAKA JANA |
Simba inajiandaa kuivaa Yanga katika mechi ya mzunguko wa pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
“Ndiyo, sasa nipo Morogoro kambini ninaendelea na mazoezi,” alisema Al Siyabi.
Al Siyabi alikuwa kimfua kipa Juma Kaseja, baadaye Ivo Mapunda na kinda Peter Manyika.
...AKIZUNGUMZA NA MHARIRI WA GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO, PHILLIP NKINI WAKATI ALIPOFANYA ZIARA KWENYE OFISI ZA GAZETI HILO. KATIKA NI MKUU WA KITENGO CHA HABARI CHA SIMBA, HAJI MANARA. |
0 COMMENTS:
Post a Comment