Kikosi cha Mbeya City kimejiongezea pointi tatu muhimu katika Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa JKT Ruvu kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo.
Mbeya City ilipata mabao yake yake mawili kupitia Hassan Mwasapili na Yohanna Morris na Mussa Juma akaifungia JKT bao moja la kufutia machozi.
Kikosi cha Mbeya City, kilisimama vema sehemu ya kiungo kikiwatumia wakongwe Haruna Moshi 'Boban', Ramadhani Chombo 'Redondo' na kinda Raphael Alfa na kuipa wakati mgumu JKT.
MBEYA CITY |
JKT RUVU |
0 COMMENTS:
Post a Comment