February 1, 2016



Na Saleh Ally
RAIS Dk John Pombe Magufuli ametuma salamu zake za pongezi kwa mshambuliaji mpya wa timu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mtanzania, Mbwana Ally Samatta.

Magufuli ambaye kitaaluma pia ni mwalimu, amefurahishwa na alipofikia Samatta. Kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa naMichezo, Nape Nnauye amewasisitiza wanasoka wengine kuichukulia ishu ya Samatta kama changamoto kwao.

Maanayake, wanasoka waongeze juhudi na maarifa kuhakikisha pia wanakuwa ni sehemu ya mafanikio hayo.

Kitendo cha rais Magufuli kukumbuka kumpongeza Samatta ni jambo jema na huenda linaongeza kuwapa nguvu wanasoka na wanamichezo wengine kuendelea kuongeza juhudi ili kufanikiwa.

Lakini kwangu naona serikali imekuwa haiweki nguvu ya kutosha katika michezo. Imekuwa ikiona michezo ni kama sehemu ya kujifurahisha na ikiwezekana si jambo kubwa sana.

Ushiriki wa viongozi wengi wa michezo umekuwa ni wakati wa kupongezana tu. Kabla ya hapo, wakati mafanikio yanatafutwa si rahisi kuwaona wakiungana na ‘wachimba’ mafanikio hadi pale inapofikia wakati wa sherehe ya upatikanaji wa madini kutokana na juhudi za wachimbaji.

Mafanikio ya Hasheem Thabeet hadi kucheza Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani (NBA), zaidi yamejaa juhudi binafsi pekee. Hali kadhalika kwa Samatta hadi anakwenda TP Mazembe ya DR Congo nasasa KRC Genk ya Ubelgiji, ni hizo juhudi binafsi.

Angalia akina Rashid Matumla na familia yao, mafanikio yao yamchezo wa ngumi. Hali kadhalika familia ya Cheka, ni watu wenye juhudi binafsi.

Hatuwezi kuendelea kukaa chini tukisubiri mtu mwingine wa juhudi binafsi ili apongezwe na viongozi mbalimbali wakiwemo wale wajuu serikalini. Badala yake serikali inapaswa kuona kwamba kuna watu wenye uwezo na vipaji na kama yenyewe itaingia na kuwa sehemu ya msukumo, basi watakaofanikiwa ni wengi sana.

Juhudi binafsi ni jambo muhimu, lakini kuna mambo yanalazimika kuguswa na serikali. Iwe kwa msukumo, kutengeneza mifumo, kanuni na sheria na hata kuingia gharama.

Kuna mtu aliwahi kuniambia, serikali imejituma na kuweza kujenga uwanja. Huo uwanja ni tokea awamu ya tatu ya Rais Benjamini Mkapa, sasa hauwezi kubaki kama nembo ya mafanikio na mfano huku serikali ikikaa kando na kusubiri mashujaa wapatikane kwa nguvu binafsi, yenyewe iingie kusherehekea tu.

Pia uwanja huo, umekuwa ukiingizia serikali fedha nyingi sana. Kupitia mchezo, uwanja huo ni mradi na inafaidika. Hivyo iwe sehemu ya mwanzo kung’amua kwamba michezo ni biashara inayoweza kuingiza pato kubwa kwa taifa.

Serikali inaweza kuisaidia michezo kuleta wataalamu. TunajuaRais wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete alionyesha juhudi kwakuwalipa makocha wa timu za taifa za soka, netiboli, mpira wa kikapu. Ahsante sana, lakini bado ilionekana ni kama juhudi binafsi, vizuri sasa liwesuala la serikali hasa ambalo linaweza kuwa na mwendelezo.

Kila mmoja anajua rais Magufuli ni imara, mwenyemisimamo, asiyetaka utani katika kazi hasakatika suala la maendeleo. Sifa hizo kama zitaigusa michezo na kwakuwa ana waziri kama Nape ambaye ana moyo wa kupambana, kunaweza kukawa na mabadiliko makubwa kwenye michezo.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo lazima iwe na wataalamu wa michezo mbalimbali. Lazima iwe na mfumo bora wa kuangalia wachezaji vijana au makinda, wakuzwe na kuendelezwa.

Mimi niwe wazi tu, nimechoshwa na kusikia watu kutoka wizarani wakisikika wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mchezo fulani, utasikia walikabidhi bendera na wakapewa shukurani nyingi kwa kufika pale.

Lakini hauwezi kusikia wakipamba na kuibadili sera yamichezo ambayo imetengenezwa miaka zaidi ya 40 iliyopita nainaendelea kubaki kuwa tegemeo hadi sasa na hakuna anayeona kama tunakwenda kwa “ndoto ya mwaka 47”, lakini watumishi wengi wa serikali wanaamini tutafika!



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic