Simba imeamua kupiga hatua kimaendeleo baada ya kuzindua rasmi duka la kuuza bidhaa zake mbalimbali.
Duka hilo linamilikiwa Insight Media ambao watakuwa wanauza bidhaa za klabu za Simba.
Duka hilo liko Dar Free Market na litakuwa likiuza vitu hivyo kwa bei nafuu na onyo limetolewa kwa wanaouza bidhaa feki.
Wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Rais wa Simba, Evans Aveva aliwashauri Wanasimba wenye uwezo kujitokeza.
“Waje nao tuwapa tenda kama hii kwa Insight, wasaidie kuuza vifaa hivi. Wao watafaidika, klabu pia itafaidika na kupata maendeleo,” alisema Aveva.
0 COMMENTS:
Post a Comment