March 27, 2016


BARUA YA CHAD

Chad imejitoa kwenye michuano ya kuwania kucheza Kombe la Afcon.


Kwa uamuzi huo, maana yake mechi kati ya Chad na Taifa Stars iliyokuwa ichezwe kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, haitakuwepo.

Maofisa wa TFF wamethibitisha kupotea taarifa hizo, lakini hata hivyo wakasisitiza si wasemaji wakuu.

"Katika hili wahusika wakuu ni Caf, hivyo tunaliacha kwa kamisaa wa mchezo ambaye ni mwakilishi wa shirikisho hilo. Yeye ndiye atatoa taarifa rasmi.

"Lakini sisi tumeelezwa kuwa Chad walikosa nauli ndiyo ikawa chanzo," kilieleza chanzo kutoka ndani ya TFF.

"Hakika haya ni masikitiko makubwa kwa kuwa wanatutishwa mzigo kwa maana ya kupokwa pointi tatu tulizowashinda ND'jamena."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic