March 27, 2016Kipa wa zamani wa Simba na Uganda ‘The Cranes’, Abel Dhaira amefariki dunia leo nchini Iceland alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mitandao mitatu ya michezo ya Uganda ukiwemo ule wa Kawowo.com imetangaza kifo cha kipa huyo aliyekuwa akisumbuliwa na kansa ya utumbo.

Dhaira amefariki akiwa na umri wa miaka 28 na Januari mwaka huu ndiyo aligundulika kuwa na ugonjwa huo.

Hadi mauti yanamkuta alikuwa bado ni kips wa IBV Vestmanaeyjar ya  Iceland.

PUMZIKA KWA AMANI DHAIRA
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV