EBOUE (KUSHOTO) AKIWA NA SALEH ALLY "JEMBE" |
Baada ya kuona sass ni maji ya shingo, hatimaye beki Emmanuel Eboue amekubali kukaa na wakala wake wa zamani na kutaka wamalizane.
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), limemsimamisha Eboue raia wa Ivory Coast baada ya kubainika alishindwa kumlipa wakala wake wa zamani, Sebastien Boisseau kitita cha pauni million moja.
Kutokana na uamuzi huo wa Fifa, ndani ya siku 22 tu tokea ajiunge na Sunderland, nayo ikaamua kumsimamisha hadi hapo atakapomalizana na wakala wake huyo wa zamani.
Lakini Kocha wa Sunderland, Sam Alladyce naye amesisitiza, Eboue amalize suala hilo ndani ya siku 14, kama akishindwa, basi hatamhitaji tena.
Boisseau amezungumza moja kwa moja na SALEHJEMBE kutoka nchini Ufaransa na kusema, Eboue beki wa zamani wa Arsenal na Galatasaray amemtaka wakutane.
“Anataka tulimalize, mimi sina shida hata kidogo. Kinachotakiwa ni kunilipa tu fedha zangu, litakuwa limeisha.
EBOUE BAADA YA KUTUA SUNDERLAND |
“Nimejaribu kuzungumza naye mara nyingi, hakusikia na wakati mwingine hakutaka hata kupokea simu,” alisema Boisseau.
“Sasa nasubiri nione atakachofanya, ninaamini atakuwa muungwana ili tulimalize salama na yeye aendelee na kazi yake.”
Juhudi za kumpata Eboue zilikwama kwa kuwa simu yake ilikuwa ikiita muda wote. Tunaendelea kumfuatilia, kama tutampata baadaye tutawaletea alichosema.
0 COMMENTS:
Post a Comment