March 9, 2016



MAYANJA


Kocha wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja amewataka maproo wa Yanga wakiwemo mastraika hatari, Donald Ngoma na Amissi Tambwe kuonyesha uwezo wao kwenye michuano ya kimataifa kwani wamesajiliwa kwa kuisaidia zaidi timu hiyo kimataifa.

Mayanja ameyasema hayo huku akifahamu kwamba Yanga wikiendi hii itacheza na APR ya Rwanda kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo utakaopigwa Kigali, Rwanda.

Yanga ina wachezaji saba wa kigeni ambao ni Wazimbabwe, Ngoma na Thabani Kamusoko, Wanyarwanda Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima, Mrundi Tambwe, Mtogo Vincent Bossou na Mniger Issoufou Boubakar.

TAMBWE

Mbali na Mayanja kuwapa majukumu hayo maproo wa Yanga, pia akawageukia wale wa Azam FC na kuwataka kutobweteka katika kuipa mafanikio timu yao.

“Katika michuano ya kimataifa, nazitakia kila la kheri Azam na Yanga ziweze kucheza vizuri na kufanikiwa kusonga mbele. Kwanza wanapaswa kujua kwamba hii ni michuano ya kimataifa na siyo ligi kuu, hivyo wanahitaji kubadilika ili kufikia malengo.

NGOMA

“Wachezaji ndiyo wanatakiwa kubadilika hasa hawa profesheno, huu ni muda wao wa kuonyesha uwezo wa hali ya juu na kudhihirisha kwamba hawakubahatisha kuja kucheza hapa nchini. Nadhani wakilitambua hilo watafika mbali sana na kuwapa raha mashabiki wao,” alisema Mayanja.

Katika hatua nyingine, Mayanja alisema kwa upande wa kikosi chake ambacho kina wachezaji saba wa kigeni, pia anakiandaa kucheza kimataifa kwani lengo lao hasa ni kushiriki michuano hiyo msimu ujao baada ya dalili za kufanya hivyo kuanza kuonekana.


“Pia wachezaji wangu nawaandaa ili wacheze kimataifa kutokana na hali halisi ilivyo kwa sasa kwenye ligi, kila timu imekuwa ikipambana kusaka ubingwa kuiwakilisha nchi, na sisi pia tupo kwenye harakati hizo, hivyo nimekuwa nikiwasisitizia wachezaji wangu kupambana kwenye hadhi ya kimataifa,” alimaliza Mayanja.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic