March 14, 2016


Mshambuliaji nyota wa Yanga, Donald Ngoma ametupia picha mtandaoni akimuonyesha mwanaume mmoja ambaye ni mlemavu na kusema anampa heshima kubwa.

Ingawa hakuweka maelezo ya kutosha, lakini Ngoma ambaye ni mpambanaji uwanjani anaonyesha kufurahishwa na namna mlemavu huyo alivyokataa mambo ya kuomba asaidiwe na badala yake amekuwa mbunivu.

Huenda ni kwao Zimbabwe, mlemavu huyo anaonekana akiuza bidhaa zake rejareja lakini akiwa nadhifu kabisa.


Picha hiyo inaweza ikawa funzo kwa wale ambao wamekata tamaa kutokana na ulemavu. Kwamba maisha yanaweza kuendelea na wakawa wafanyabiashara wanaoweza kuendesha maisha yao wenyewe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV