March 29, 2016


Uganda imekubali sare ya bila bao katika  mechi kuwania kucheza Afcon.
Sare hiyo ni dhidi ya Burkina Faso katika mechi iliyochezwa mjini Kampala, Uganda, leo.

Licha ya juhudi za washambuliaji wake, Emmanuel Okwi na wenzake, lakini hawakuweza kuifungia Uganda bao.


Hata hivyo, Uganda walifanya mashambulizi mengi zaidi lakini wakashindwa kuzitumia nafasi walizozipata.

Katika mechi iliyopita, Uganda ililala kwa bao 1-0 ikiwa ugenini dhidi ya Burkina Faso.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV