March 29, 2016


Nimeikuta picha hii katika makabla yangu, niliipiga mwaka 2009 nchini Iviry Coast wakati Tanzania ikishiriki katika michuano ya Chan.

Mabeki Salum Sued na Kelvin Yondani walichaguliwa na kuwa waliotakiwa kwenda kupimwa kama wanatumia dawa haramu za kuongeza nguvu.

Huu ulikuwa ni utaratibu wa kila mechi, wachezaji wawili wa kila timu wanachukuliwa kwenda kupimwa.

Nakumbuka siku moja, Mrisho Ngassa alikuwa majeruhi, akawa amekaa jukwaani. Lakini akachukuliwa kwenda kupimwa.

Kidogo tulishangaa, lakini mfumo ulikuwa unaruhusu hilo kufanyika. Kwani ili wapatikane wawili wanaotakiwa kupimwa siku hiyo, majina ya wachezaji wote yanaingizwa kwenye chungu au boksi halafu mhusika anachagua mawili.


Hivyo wakati Ngassa wakati anachaguliwa alikuwa jukwaani, lakini akaenda kupimwa. Kitu kizuri kabisa, wachezaji wote wa Tanzania waliokuwa wakipimwa, wote walibainika kuwa “safi kabsaaaaaa.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV