March 17, 2016Simba imeanza safari ya kwenda Tanga kuwavaa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano cha Simba, Haji Manara amesema wameishaanza safari.

“Tayari tumeanza safari ya kwenda Tanga, kila kitu kinakwenda vizuri. Tunamuomba Mungu atusaidie tufike salama,” alisema Manara.


Tayari Simba imetangaza mechi dhidi ya Coastal Union itakuwa ya mwisho, halafu itapumzika hadi wengine yaani Yanga na Azam FC, wacheze viporo vyao vitatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV