Baada ya kurejea nchini usiku wa kuamkia leo, Taifa Stars imeendelea na mazoezi yake leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Stars imefanya mazoezi jioni hii kuendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi ya pili dhidi ya Chad. Stars ilipata ushindi wa bao 1-0 ikiwa ugenini Chad.
Mazoezi ya leo yalionekana kwenda vizuri huku wachezaji wa Stars wakionekana kutokuwa na uchovu licha ya safari ndefu kutoka ND’jamena.
Kikosi cha Stars kitashuka dimbani Taifa Jumatatu kuwava Chad katika mechi yake ya nne ya kundi G.
0 COMMENTS:
Post a Comment