March 25, 2016

Beki Kelvin Yondani na kiungo Mwinyi Kazimoto wameonekana wakiwa jukwaani wakati kikosi cha Taifa Stars kikiendelea na mazoezi yake leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.

Stars imefanya mazoezi jioni hii kuendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi ya pili dhidi ya Chad. Stars ilipata ushindi wa bao 1-0 ikiwa ugenini Chad.

Lakini Kazimoto aliyeumia katika mechi iliyopita na Yondani iliyeelezwa ni majeruhi walikuwa kama watazamaji jukwaani.


Kikosi cha Stars kitashuka dimbani Taifa Jumatatu kuwava Chad katika mechi yake ya nne ya kundi G.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV