March 15, 2016


Mshambuliaji nyota wa Yanga, Amissi Tambwe amerejea mazoezini baada ya kusumbuliwa na enka iliyosababisha acheze kipindi kimoja katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya APR jijini Kigali, Jumamosi.

Tambwe ameanza kujifua na wenzake kwenye Viwanja vya Polisi barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Tambwe alisema ameanza mazoezi baada ya kupata nafuu.

“Sasa nina nafuu, angalau nimeanza mazoezi na wenzangu. Nitaendelea hivi, matumaini yangu hadi mechi na APR nitakuwa vizuri,” alisema Tambwe.

APR itakuwa Dar es Salaam kuwavaa Yanga Jumamosi katika mechi ya marudiano baada ya kuchapwa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza.


Tambwe raia wa Burundi, tayari ana mabao 50 aliyofunga kwenye Ligi Kuu Bara katika misimu miwili na nusu kati ya hayo 20 amefunga akiwa Simba na 30 akiwa na Yanga. Mabao haya ni upande wa Ligi Kuu Bara tu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV