April 20, 2016


Yanga wamepambana mpaka dakika ya 95+ ndipo wakaruhusu bao la pili, hivyo mchezo umamlizika wamfungwa mabao 2-1, wanatolewa kwenye michuano kwa jumla ya mabao 3-2.

Mwamuzi anamaliza mchezo.

Dakika ya 95+: Al Ahly wanapata bao baada ya mfungaji kupiga krosi kutoka upande wa kulia na kuunganishwa kwa kichwa.
 
Dakika ya 94+

Dakika ya 92+ Matokeo bado 1-1

Dakika ya 90: Zimeongezwa dakika 5 za nyongeza.

Dakika ya 89: Mchezo umechangamka, benchi la Al Ahly wote wanaonekana hawaamini kile kinachotokea uwanjani.

Kipa wa Yanga, Dida amefanya kazi nzuri, ameokoa mara mbili hatari zilizokuwa zikiingia wavuni.

Dakika ya 87: Al Ahly wanafanya shambulizi la nguvu.
 
Dakika ya 85: Deus Kaseke ametoka, ameingia Kelvin Yondan.

Beki wa Yanga, Bossou alikuwa mstari wa mbele kuwavuruga wachezaji wa Ah Aly ambao wanaonekana kupaniki na kutaka kuwavuruga Yanga.

Dakika ya 83: Mchezo unaendelea, Ngoma na mchezaji moja wa Ah Aly wanapewa njano kila mmoja.
 
Dakika ya 81: Mchezo umesimama wachezaji wa Yanga na wa Al Ahly wanatibuana, mwamuzi anaingilia lakini bado mpira umesimama.
 
Dakika ya  80: Vurugu zinatokea uwanjani.

Dakika ya 77: Deus Kaseke yupo chini ameumia, mchezo umesimama.

Dakika ya 76: Mchezo bado ni wa kushambuliana kwa zamu.


Dakika ya 73: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Tambwe anaingia Malimu Busungu

Yanga wanaonekana kuamka na kucheza vizuri.

Dakika ya 69: Yanga wanafanya mashambulizi makali.

Dakika ya 66: Yanga wanasawazisha, kazi nzuri iliyofanywa na beki wa kulia Juma Abdul, anamtoka beki wa Al Ahly, anapiga krosi inayotua kichwani mwa Donald Ngoma anafunga bao zuri.

Mfungaji wa bao la AL Ahly ni Hossam Ghaly

Dakika ya 62: Yanga wanatulia na kupiga pasi za kuonana hasa katikati ya uwanja.

Dakika ya 61: Yanga wanatulia wanapanga mashambulizi vizuri, Msuva anashidwa kutumia nafasi akiwa ameshamtoka beki wa mwisho, baadaye anazidiwa kasi, anayang'anywa mpira.

Dakika ya 58: Al Alhy bado wanashambulia kwa kasi, mashabiki wanashangilia kwa nguvu.

Dakika ya 56: Dida anapangua shuti kali la Al Ahly, mpira unakuwa kona.

Dakika ya 55: Bao lilipatikana baada ya kupiga kichwa mpira wa kona ambao ukaingia moja kwa moja wavuni



Dakika ya 51: Al Ahly wanapata bao kutokana na mpira wa kona.

 
Dakika ya 49: Al Ahly wanakosa bao, mpira unakuwa kona.

Dakika ya 47: Al Ahly 0, Yanga 0

Kipindi cha pili kimeanza.

Matokeo ni 0-0


Dakika 45: Zimekamilika mchezo ni mapumziko.

 Dakika 45: Zinaongezwa dakika 2

Dakika ya 44: Al Ahly wanacheza soka la kasi muda mwingi lakini Yanga wanapambana nao kuwapunguza kasi.


Dakika ya 42: Yanga wanapata kona ila mwamuzi anakataa kuwa siyo kona.


Dakika ya 40: Kipa Dida anadaka shuti kali.


Dakika ya 38: Mashabiki wa Al Ahly wanammulika Dida na miale usoni ili kumpoteza dira.



Kama Bossou angechelewa kidogo kuutoa mpira huo mshambuliaji wa Waarabu alikuwa ameshafika na angefunga.


Dakika ya 34: Al Ahly wanapiga shuti kali Dida anapangua lakini Bossou anafanya kazi nzuri anauwahi mpira anautoa nje inakuwa kona.


Dakika ya 30: Mchezo unaendelea, Dida amenyanyuka



Dakika ya 28: Dida anaendelea kutibiwa, mchezo umesimama kwa muda.


Dakika ya 27: Ah Ahly wanapata kona inapigwa, wanamfanyia faulo Dida, mwamuzi anapuliza kipenga. Dida bado yupo chini.


Dakika ya 25: Mashabiki wa Al Ahly wanashangilia kwa nguvu hapa uwanjani.


Dakika ya 22: Ah Aly wanafanya mashambulizi ya nguvu lakini mipira yote imetoka nje.


Dakika 17: Kamusoko anapiga faulo mpira unapaa juu ya lango na kutoka nje.


Dakika ya 16: Yanga wanapata faulo nje ya lango la Al Ahly

Wachezaji ndiyo wanaingia uwanjani, kipindi cha pili kinakaribia kuanza.

Dakika ya 14: Yanga wanacheza vizuri wanapigiana pasi katikati ya uwanja, msuva anaondoka na mpira lakini anapiga pasi hovyo, kipa wa Al Ahly anauchukua mpira.


Dakika ya 12: Mchezo bado umebalansi, timu zote zinacheza soka la pasi.



Wachezaji wa akiba wa Yanga
Barthez, Telela, Yondan, Nonga, Busungu, Twite na Aboubakar


Kikosi cha Yanga

Dida
Juma Abdul
Oscar Joshua
Nadir Haroub
Vicent Bossou
Thaban Kamusoko
Simon Msuva
Haruna Niyonzima
Donald Ngoma
Amiss Tambwe
Deus Kaseke


Dakika ya 7: Al Ahly wanapiga kona inatoka nje.


Dakika ya 6: Al Ahly wanafanya shambulizi kali, kipa wa Yanga, Dida anapangua inakuwa kona.


Dakika ya 5: Ah  Ahly wanamiliki mpira muda mwingi. Taarifa zaidi juu ya vikosi inakuja.


Dakika ya 3: Matokeo bado 0-0

Dakika ya 1: Mchezo ndiyo umeanza.








0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic