April 22, 2016

KIPA wa Simba, Vincent Angban, raia wa Ivory Coast, amefunguka juu ya taarifa kuwa alimpiga ngumi beki wa timu yake, Hassan Kessy mara baada ya timu hiyo kufungwa bao 1-0 na Toto Africans, Jumapili iliyopita.
ANGBAN (WA PILI KUTOKA KULIA)

Angban amesema kuwa hakufanya tukio hilo, bali walipishana kauli tu na kuwa alimkunja, tukio ambalo lilitokea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

“Unajua kwenye maisha ya soka mambo kama hayo yanatokea na ni kawaida kwa wachezaji kugombana, unaweza kuona hata klabu kubwa duniani wachezaji wanagombana lengo likiwa ni moja tu, kuwekana sawa kwa ajili ya maslahi ya timu.

KESSY ALIPOKUWA AKIPEWA KADI NYEKUNDU

“Siku hiyo wakati tunaongea na Kessy baada ya kupoteza mchezo ikatokea kutoelewana na ndiyo yakatokea hayo yote, nadhani hakuna kibaya nilichokifanya, bali ilikuwa ni sehemu ya kuitetea timu,” alisema Angban.


Katika mechi hiyo, Kessy alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumfanyia faulo straika wa Toto, Edward Christopher ‘Edo’, kitendo ambacho uongozi wa klabu yake pia umekilaani na kumfungia kucheza mechi tano zinazofuata ambazo zinamaanisha hataichezea tena Simba msimu huu.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV