April 27, 2016

Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limetangaza kuwa Coastal Union imepoteza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga baada ya washabiki wake kuwa chanzo cha mwamuzi kuvunja mchezo huo uliofanyika Aprili 24, 2016 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Mashindano ya TFF iliyokutana leo (Aprili 27, 2016) jijini Dar es Salaam kwa kuzingatia Kanuni ya 28(2) ya Kombe la Shirikisho. Wakati mechi hiyo inavunjwa, Yanga ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1.

Pia Coastal Union imepigwa faini ya shilingi 2,000,000 (milioni mbili) kwa kuzingatia Kanuni ya 42(26) ya Ligi Kuu kutokana na vitendo vya vurugu za washabiki wake wakati wa mechi hiyo. Pia TFF haitasita kufungiwa uwanja huo iwapo vitendo hivyo vya vurugu za washabiki havitakoma.

Mwamuzi wa mchezo huo, Abdallah Kambuzi amefungiwa mwaka mmoja wakati Mwamuzi Msaidizi namba mbili Charles Simon ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi. Adhabu hizo zimetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 38(1) ya Ligi Kuu.Mchezaji Adeyum Ahmed wa Coastal Union anapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa ajili ya hatua zaidi kutokana na kitendo chake cha kumpiga kichwa mwamuzi wa akiba baada ya kutolewa nje. Hata hivyo, Ahmed hakufanikiwa kutimiza azma hiyo baada ya mwamuzi huyo kumkwepa.

Yanga imepigwa faini ya shilingi 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu kutokana na kutoingia vyumbani kwenye mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho.

Vilevile malalamiko ya Coastal Union kutaka mechi hiyo irudiwe yametupwa baada ya Kamati ya Mashindano kubaini kuwa hayana msingi wowote.4 COMMENTS:

 1. Naimani marinzi marengo yake yamekamilika ala ipo. Siku

  ReplyDelete
  Replies
  1. KI VIPI?KWANI MUAMUZI NI MALINZI PEKE YAKE MPAKA USEME MALENGO YAKE YAMETIMIA?ANGALIA SANA UANDISHI WAKO,VINGINEVYO HAYA MAANDISHI YAKO YATAKUFUNGA SIKU MOJA,'IPO SIKU'UNA MAANA GANI?OMBA MUNGU MALINZI ASIPATE TATIZO LOLOTE.

   Delete
 2. Mwenyekiti wa kamati alikuwa Kaborou, sasa Malinzi anahusikaje!?

  ReplyDelete
 3. Hawa wanaosema Yanga wanabebwa ndio maana hawafanyi vizuri kwenye mashindano ya kimataifa wanataka timu gani sasa ichukue ubingwa ili ilete kombe la kimataifa?Kwa mara ya mwisho simba kushiriki klabu bingwa Africa mwaka 2013 ilifungwa na Libolo goli 1-0 Dar es Salaam na 4-0 Angola,kumbuka Simba ilipata nafasi hiyo baada ya kuifunga Yanga 5-0 mwaka 2012 na kuchukua ubingwa.Je mnataka kutuaminisha kwamba Simba hiyo haikustahili kushiriki mashindano hayo sababu ilibebwa na TFF? Timu zote za nchi wanachama wa CECAFA zimeondolewa kwenye hatua za mwanzo na Yanga ndio iliofika 16 bora,je timu zote hizo zilibebwa na TFF zao kuchukua ubingwa ndio maana hazikufanya vizuri kwenye klabu bingwa Afrika?Na timu za Uingereza zinazochukua ubingwa wa EPL mbona hazifanyi vizuri kwenye ubingwa wa Ulaya,je na zenyewe huwa zinabebwa kwenye kuchukua ubingwa wa England?Wabongo tuache visingizio tukubali matokeo uwanjani.Kama Coastasl Union ilikuwa nzuri zaidi ya Yanga ingefunga magoli na refa angeyakubali kama alivyokubali goli lao la kwanza.Hao wanaosema Yanga ilizidiwa watuambie Timu inayozidiwa uwnjani inapata wapi nafasi ya kufunga magoli yenye utata huku ile inayodaiwa kuizidi ikishindwa kupata nafasi za kufunga angalau magoli yakataliwe na refa?Je Yanga ilizidiwa kwa kufunga magoli yenye utata au kwa Coastal kufunga magoli ambayo refa aliyakataa?kwa wale washabiki wa Simba waelewe kwamba malalamiko yao na matusi kwenye mitandao dhidi ya Yanga hayawezi kuisaidia Simba kupata ubingwa,kwani sio Yanga inayosababisha Simba ivurunde kwenye ligi hivyo wayaelekeze kwa viongozi wao waliowachagua kwa ahadi ya kuwapatia pointi tatu tatu

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV