April 22, 2016MASHABIKI WA SIMBA KWENYE UWANJA WA TAIFA LAKINI SIYO HAWA WALIOKESHA BAA WAKISHANGILIA.

USHABIKI wa soka una mambo si kitoto! Muda mfupi baada ya Yanga kuaga mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa na Al Ahly, juzi, mashabiki wa Simba waliamua kuchangishana na kwenda baa kukesha kwa ajili ya kusherehekea kipigo cha Yanga.

Mashabiki hao ambao walikuwa wakiufuatilia mchezo huo katika TV, walikuwa wakishangilia kama wapo uwanjani kwa muda wote huku wale wa Yanga nao wakiishangilia timu yao. Ilikuwa ni maeneo ya Mbogella Pub, Usangu Chimala.

Mara baada ya mechi hiyo kumalizika, mashabiki hao ambao hawakuwa tayari kujitambulisha, walisema kipigo hicho kimewapunguza machungu ya Simba kufungwa na Toto, Jumapili iliyopita katika Ligi Kuu Bara.

“Tuna furaha kubwa sana hapa tulipo, Yanga wangeshinda leo basi tungehama mjini, maana tungepewa maneno ambayo kama si mvumilivu unaweza kupigana, kuanzia kwa huyo Jerry Muro (Msemaji wa Yanga) mpaka kwa mashabiki wao, kwa matokeo haya kidogo tutapumzika,” alisema shabiki mmoja.

Wengine walionekana kuwa na furaha huku kila mtu akizungumza lake pamoja na ubishi wa hapa na pale dhidi ya wale wa Yanga.


SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV