April 22, 2016

LICHA ya Yanga kufungwa mabao 2-1 na Al Ahly ya Misri kisha kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika juzi jijini Alexandria, straika, Donald Ngoma ameweka rekodi ya kipekee.

YANGA Vs AL AHLY

Straika huyo wa Yanga ambaye ni raia wa Zimbabwe, aliweka rekodi hiyo ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Yanga kufunga bao ndani ya dakika 90 tangu timu hizo zikutane zaidi ya mara nne nchini humo lakini pia kwa timu za Misri na Uarabuni, Yanga imekuwa ikipata tabu inapokuwa ugenini dhidi ya timu za ukanda huo.

Rekodi zinaonyesha kuwa mara ya mwisho kwa mchezaji wa Yanga kufunga bao ndani ya dakika 90 ilipocheza ugenini dhidi ya timu ya Misri na zile za ukanda huo kwa jumla ni mwaka 1992, ambapo Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Ismailia jijini Cairo.

YANGA Vs AL AHLY

Pamoja na sare hiyo, bado Yanga iliondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa mwaka huo kwa kuwa katika mchezo wa awali Ismailia ilishinda mabao 2-0 jijini Dar.


YANGA Vs ETOILE DU SAHEL

YANGA VS ETOILE DU SAHEL
Katika mchezo wa juzi, Ngoma alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 57, lakini furaha yao hiyo ilikatishwa na bao la pili kwa Al Ahly lililofungwa katika dakika ya 95 ikiwa ni dakika ya mwisho katika zile za nyongeza.

Al Ahly na Yanga zimekutana mara nne nchini humo. Mara ya kwanza Yanga walifungwa 5-0, mara ya pili 4-0, ya tatu 1-0 na juzi walifungwa 2-1.

REKODI ZA YANGA KWA WAARABU

LIGI YA MABINGWA AFRIKA 1982
Raundi ya pili:
Al Ahly 5-0 Yanga
Yanga 1-1 Al Ahly

LIGI YA MABINGWA 1988
Raundi ya Kwanza:
Yanga 0-0 Al Ahly
Al Ahly 4-0 Yanga

LIGI YA MABINGWA 1992
Raundi ya kwanza:
Yanga 0-2 Ismailia
Ismailia 1-1 Yanga (Cairo)

LIGI YA MABINGWA 1998
Hatua ya makundi (Kundi B)
Raja Casablanca 6-0 Yanga (Morocco)
Yanga 3-3 Raja Casablanca

LIGI YA MABINGWA 2007
Raundi ya pili:
Esperance 3-0 Yanga
Yanga 0-0 Esperance
(Yanga iliangukia Kombe la Shirikisho, ikatolewa na El Merrekh ya Sudan kwa jumla ya mabao 2-0) 
KOMBE LA SHIRIKISHO 2008
Raundi ya kwanza:
Al Akhdar 1-0 Yanga (Libya)
Yanga 1-1 Al Akhdar

LIGI YA MABINGWA 2009
Raundi ya kwanza:
Al Ahly 3-0 Yanga
Yanga 0-1 Al Ahly

LIGI YA MABINGWA 2012
Raundi ya kwanza:
Yanga 1-1 Zamalek
Zamalek 1-0 Yanga

LIGI YA MABINGWA 2014
Raundi ya kwanza:
Yanga 1-0 Al Ahly
Al Ahly 1-0 Yanga (Yanga ilitolewa kwa penalti 4-3)

KOMBE LA SHIRIKISHO 2015
Raundi ya pili:
Yanga 1-1 Etoile du Sahel
Etoile du Sahel 1-0 Yanga
LIGI YA MABINGWA 2016
Yanga 1-1 Al Ahly
Al Ahly 2-1 Yanga


SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV