April 11, 2016


Siku chache baada ya timu ya Geita Gold kushushwa daraja, kocha wa timu hiyo, Selemani Matola ameweka wazi kuwa ataachana na timu hiyo iwapo rufaa yao haitafanikiwa.

Geita Gold inayonolewa na Matola imeingia katika kashfa ya upangaji wa matokeo kufuatia kufunga mabao 8 katika mechi ya mwisho ya Ligi Daraja la Kwanza ambapo Polisi Tabora ilifunga mabao saba, hivyo kujikuta zikishushwa hadi Ligi Daraja la Pili.

Matola amesma kuwa, anasubiri maamuzi ya rufaa yao ili ajue aamue kama ataendelea iwapo ikiamuliwa kupanda daraja au aachane nayo iwapo maamuzi ya kushushwa daraja yataendelea.

“Mimi kazi yangu tayari nimeshaikamilisha, mara baada ya ligi kumalizika tulitegemea TFF wangetutendea haki lakini wametususa, kwa sasa nasubiria viongozi wangu ambao wamekata rufaa, hivyo nasubiria kuona maamuzi yatakuwaje.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV